Friday, November 20, 2015

Wizkid afanya mahojiano na jarida la Fader la Marekani, azungumzia kumuandikia wimbo Rihanna, collabo na Chris Brown na Album yake mpya

 
Staa wa Nigeria, Ayo Balogun aka Wizkid ni mmoja ya wasanii wa Afrika ambao wanafanya vizuri kimataifa kwasasa.

Wizkid-OnoBello (3)
Wizkid amefanya mahojiano na Jarida la Fader la Marekani ambapo amezungumzia mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia muziki ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kushirikiana na muimbaji wa kundi la Cold Play, Chris Martin kuandika wimbo wa Rihanna, Collabo yake na Tinie Tempah, na wimbo ambao bado hajatoka ‘African bad girl’ aliomshirikisha Chris Brown.


Kuhusiana na Tuzo, Wizkid amesema hakuupenda muziki kwasababu ya tuzo na mashabiki wake wa kweli wanajua
“My real fans know I am not really about that kind of thing. That was not the reason why I fell in love with music”

Kuhusiana na wimbo wake wa ‘Ojuelegba’ Wizkid amesema kuwa alifahamu kuwa ni wimbo mzuri lakini hakutegemea kama ungetoboa kiasi hiki
“I knew it was a good song but I didn’t expect it to blow up the way that it did. My parents still live there. We have a house there.”
Kuhusiana na Album yake mpya aliyoipa jina la ‘The sound from the other side, Wizkid amesema
“I’m a perfectionist. I can listen to the music now and tomorrow I’ll be like, ‘Yo, I feel we need to change this’, and then we have to go back to the drawing board”
F101_GENF_WIZKID_WILTON_06_WEB_oqgvkq
Jarida la Fader ni moja ya majarida makubwa marekani, baadhi ya matoleo yaliyopita ni pamoja na toleo la Drake na Rihanna.

No comments: