areed kuband aka Fid Q amesema kitendo cha ‘engineer’ wa muziki
kutoka Afrika Kusini kumuita “Underground” wakati wa wa soundcheck ya
show ya Wizki kimempa changamoto za kufanya jitihada zaidi ili aweze
kufika hatua ya kujulikana kimataifa.
“Mimi na bendi yangu tulifika pale mapema kwa ajili ya
masuala ya Sound Check, kwanza ilitangulia bendi yangu wakawa
wanazungushwa sana kufanya sound check, ikabidi niende mwenyewe, jamaa
akaniambia mtafanya sound check, mi ikabidi nimfuate jamaa nikamwambia
vipi mbona sisi tumefika mapema lakini hatufanyi sound check, akaniambia
take it easy man, those guys with big names they deserve to do sound
chek alafu nyinyi ma underground mtafuatia” Fid Q ameiambia Planet Bongo
Aliongeza kuwa japo alicheka lakini kitendo icho kimempa changamoto kubwa ya kuhakikisha anajulikana kimataifa “Basi
mi na bendi yangu tukabaki tunacheka tukaipenda, bendi yangu ikaniuliza
unajisikiaje kuhusiana na hicho kitu!? nikasema jamaa kanifurahisha kwa
sababu ye anajua watu ambao anawaona katika TV za kimataifa, wengine
sisi hatuonekani kwa hiyo kanikumbusha mi bado nina localy, kwa hiyo
nina kazi kubwa ya kujipromote kimataifa, kwa hiyo nimechukulia kauli
yake kama challenge na jamaa hajakosea” Alisema Fid Q.
No comments:
Post a Comment