Msanii Wa Kike Wa Humu Nchini AKOTHEE, Hivi Majuzi Aliachia Kazi Yake
Mpya ambaye amemshirikisha gwiji wa Afrika Mashariki DIAMOND PLATNUMZ
Inayokwenda Kwa Jina 'Sweet Love'. Akizungumza na Mzazi Willy M TUVA
Kupitia Kipindi Cha #MamboMseto
Ya Radio Citizen, Msanii Huyo Alifunguka Kuwa Kazi Hiyo ilichukua siku
mbili Kurecord "Sweet Love

ilituchukua Siku Mbili Kurecord, Tulianza
Kurecord Kwanzia Saa Tatu Usiku Hadi Saa Kumi Na Moja na Producer LIZA
kwenye studio za WCB" Alisema Akothee. Kuhusu Swala La Hela Kama
alimlipa Diamond Platnumz Kufanya Naye Kazi, Akothee alikuwa na Haya ya
Kusema " Muziki ni biashara, na kila mtu akifanya biashara lazima aone
matokeo ama inaitwa profit ,na ngoma imetoka kwa ivyo tushughulikie
audio na video. Swala La Hela Hilo tusiingilie, maanake mara nyingi
nikitaja kitu tu watu wanakasirika wanaanza kusema mbona hakutumia hiyo
sijui kuenda kufanya nini " alimazia AKOTHEE.
No comments:
Post a Comment