Wednesday, March 16, 2016

Baraka da Prince aelezea sababu za kutofanyika kwa Collabo zake na Eddy Kenzo na Patoranking

Baraka da Prince aliwahikutangaza ujio wa collabo zake kubwa na msanii wa Uganda, Eddy Kenzo na msanii wa Nigeria, Patoranking lakini hazikuwahi kutokea.
Muimbaji huyo wa ‘Siwezi’ amedai sababu za kutofanyika kwa collabo hizo ni kwasababu alibadilisha uongozi wake
 
“Ni kweli Collabo zilitakiwa zifanyike lakini sema baada ya kuwa na uongozi mpya sikuweza kufanya collabo na Eddy Kenzo na Patoranking hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa na kila kitu kilikuwa kimefanyika kilichobaki ni mimi tu kufanya nao sema kilichosababisha ni kuwa na uongozi mpya kwani uongozi wa zamani ndio walikuwa wamepanga collabo hizo”

No comments: