Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya
vizuri na wimbo wake wa 'Ndi ndi ndi' amefunguka na kuweka wazi wazi
msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi.
Msanii Lady Jaydee
Kupitia Accout yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka
kwa mashabiki zake Lady Jaydee aliulizwa swali kama ataweza kufanya
remix ya wimbo wake mpya na kama atafanya hivyo anadhani ni msanii gani
wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa
sasa anamfikiri sana Mr Blue.
"Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri
zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue"
alisisitiza Lady Jaydee
Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye
muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu
wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001
yeye si mtu ambaye anatoka ngoma mara kwa mara bali huwa anajipa muda ya
kujiandaa lakini hata hivyo nyimbo anazokuwa anatoa zinadumu muda mrefu
ndiyo maana anakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku.
"Ndio utaratibu niliojiwekea miaka yote tangu Album ya kwanza 2001, mimi
huwa sio msanii wa back to back lakini uzuri nyimbo zenyewe hudumu
miaka mingi hivyo nakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku.
Zitakapoisha nyimbo zilizomo kwenye album hii ya 7 itachukua muda tena
kutoa zingine. Huwa najiandaa" alisema Lady Jaydee
Baadhi ya mashabiki walitaka kufahamu msimamo wake juu ya wasanii
kutumia vilevi na madawa ya kulevya na ndipo hapo Lady Jaydee aliposema
kuwa ni sawa kutumia dawa za kulevya ila hyaina ubaya kwa msanii au mtu
kutumia kilevi kidogo na kusema ili mradi usiwe kero kwa watu wengine.
"Si sawa kutumia dawa za kulevya ila haina ubaya kujichangamsha na Lager
kiasi ilimradi usikere watu wengine. Vilevi vinatofautiana vipo
visivyofaa vyenye madhara, si halali, situmii. Natumia halali Kama Wine
na Beer". Lady Jaydee.
No comments:
Post a Comment