Meneja wa kundi la Yamoto Band na diwani wa
kata ya Kirungule amefunguka na kusema kuwa Kayumba Juma mshindi wa
shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search (BSS)
amemaliza pesa yake milioni 50 na kusema katika vitu alivyofanyia na
hela hiyo ni pamoja na kununua gari. Akizungumza kwenye eNEWS Said Fella
amedai kuwa walimnunulia gari msanii huyo kutokana na kazi yake hiyo ya
sanaa pamoja
na jinsi ambavyo jamii inamchukulia msanii huyo hivyo
uamuzi wa kumnunulia gari ulikuwa ni uamuzi sahihi. "Kwa pesa alizopata
Kayumba zile milioni 50 amenunua gari na zingine amejenga hilo banda au
nyumba ndiyo maana hata hiyo finishing ya nyumba atafanya baada ya
kuanza kupata show, ila zile milioni 50 ziliisha. Mwisho wa siku
anajenga nyumba kwa hela yake siyo kujenga nyumba kwa hela aliyotunzwa
na mtu, kwa
hiyo lazima sanaa yake imsababishie kujenga nyumba
inayofanana na yeye na maisha yake". alisema Said Fella "Tukisema
kwanini alinunua gari na si kujenga nyumba hilo nalo ni kosa, yule ni
msanii hivyo angepanda daladala mngesema kuwa kwanini amepanda daladala
unajua nyumba siku zote haionekani" alisisitiza Said Fella.
No comments:
Post a Comment