Video ya wimbo
mpya wa ‘Namjua’ wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nurdin Bilali
‘Baba Qayla’ au ‘Shetta’, iliyofanyiwa jijini Johannesburg na Cape town
nchini Afrika Kusini, inatarajiwa kuachiwa kesho katika vituo mbalimbali
vya runinga. Uwekezaji katika video hiyo umekuwa mkubwa kwani
zimetumika
ndege, boti na nyumba za kukodi zilizogharimu kiasi kikubwa
cha fedha ili kuvutia na kujiongeza katika soko la kimataifa. Shetta
alisema ametumia siku nne kurekodi wimbo huo baada ya wiki mbili za
kusaka na kupata mandhari nzuri zinazoonekana katika video hiyo. “Video
hii nimewekeza vya kutosha maana hadi wasichana ‘video queens’
waliotumika humo ni wa kimataifa. Video yenyewe inaelezea mambo
mbalimbali ikiwemo mapenzi na ufahari katika mambo mbalimbali, imani
yangu itanifikisha kimataifa zaidi,” alieleza Shetta. Video hiyo
imerekodiwa chini ya studio ya WCB na mtayarishaji kutoka kisiwani
Comoro, Jobanjo akishirikiana na prodyuza, Laizer kutoka studio hiyo.
No comments:
Post a Comment