Msanii wa Bongo Fleva, Abdu Kiba amefafanua kauli yake aliyoitoa kwenye kipindi cha Planet Bongo kuwa yupo tayari kufanya kazi na label ya WCB iwapo watakubaliana.
“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” Chid Benz alifunguka kwenye kipindi icho.
Abdu kiba ameibuka kuifafanua kauli hiyo ambapo amedai kuwa watu walimuelewa vibaya lakini hakuwa na maana hiyo,
“Mimi nina label yangu, nina label inayosimamia kazi zangu, inasimamia muziki wangu, Inasimamia kila kitu changu” Abdu Kiba ameiambia AyoTv “Nashangaa taarifa ambazo zinanifika tofauti, kutoka kwa mashabiki, kutoka kwenye blogs tofauti like kwamba Abdu Kiba anasema anaweza kukaa mezani na kusaini sijui label sijui ya nini nini No, siwezi kufanya hivyo kwasababu nina label yangu, Ila labda wakati naongea lile neno watu walinielewa tofauti” Abdu Kiba alifafanua.
Abdu Kiba amesema yeye yupo tayari kushirikiana kwenye kazi tu lakini sio kuama label.
No comments:
Post a Comment