Sio watu wote waliofurahia Rich Mavoko kusainiwa chini ya label ya WCB, ikiwemo wasanii wengine wakubwa wa Bongo Fleva.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, Mavoko amedai kuwa kuna msanii alimkataza kusainiwa chini ya label hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz baada ya taarifa za yeye kusainiwa kwenye label hiyo kutoka.
“Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz ” Mavoko alifunguka. “Kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu.”
Rich Mavoko tayari ameachia wimbo wa kwanza akiwa chini ya label hiyo, Ibaki Story
No comments:
Post a Comment