Kwa mwanaume baraka kutoka kwa mke wake zina nguvu mno hasa kwakuwa maandiko matakatifu yanasema kuwa mwanamke alitokana na ubavu wa mwanaume. Mrs Nasib Abdul, Zari amempa baraka zake mpenzi wake Diamond ambaye amesafiri kwenda Los Angeles, Marekani kwenye tuzo za BET. Diamond ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.
“Safari njema. May the Good Lord be with you all the way. Praying you bring the BET Award back to East Africa…. xoxo @diamondplatnumz,” ameandika Zari kwenye Instagram.
Hata hivyo kipengele hicho kina upinzani mkubwa mwaka huu. Msanii pekee ambaye ni tishio kwa Mond ni Wizkid. Staa huyo wa Nigeria mwaka huu amefanya mambo makubwa ikiwemo kushirikishwa na Drake kwenye wimbo ‘One Dance’ ulioshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa wiki sita mfululizo. Pia amezunguka na Chris Brown kwenye ziara yake ya One Hell of A Nite’ barani Ulaya.
Wasanii wengine wanaowania kipengele hicho ni AKA, Cassper Nyovest, Yemi Alade na wengine.
No comments:
Post a Comment