Kama umeingia Twitter dakika kadhaa zilizopita, utakua umekutana na trending story juu ya single mpya ya rapa na DJ maarufu kutoka nchini Marekani, namzungumzia DJ Khaled aliyeachia single yake ya nne iitwayo "Do You Mind" yenye collabo ya mastaa kama Nicki Minaj, Chris Brown, August Alsina, Jeremih, Future na Rick Ross. Wimbo huu mpya wa DJ Khaled umeachiwa rasmi na uko kwenye playlist ya radio stations nyingi duniani na inapata positive feedback.
Muda mchache baada ya kuachiwa kwa single hiyo, umezuka mjadala kwenye forum ya KTT ulioanzishwa na jamaa anayejiita Foreign a.k.a. Foreign Beats
akimtuhumu DJ Khaled kuiba beat yake. Jamaa kaenda mbali zaidi, kwa kuipload instrumental yake kupitia YouTube ambayo alitengeneza tangu mwezi January na kuipa tittle ya "DJ Khaled Type Beat 2016 x Chris Brown x Future - Friends | Prod. by Foreign Beats." Bonyeza Link Kuisikiliza Beat Hiyo.
Wapo baadhi ya watumiaji wa mtandao wa KTT ambao wanaufananisha wimbo mpya wa DJ Khaled na sample za wimbo wa muiambaji Usher " Lovers & Friends." Sasa kama ukijaribu kusikiliza nyimbo hizo mbili pamoja na beat ya mlalamikaji kuna ladha fulani za kufanana, pia ukioongeza na jina la beat ya producer Foreign ni kama zinampa nguvu mtayarishaji huyo.
Pamoja na kilichotokea, bado haitakua fair kumuita DJ Khaled ni mwizi, that's why nahitaji comment yako juu hili.
Imeandikwa na: David King (Programs Director - Kings FM)
No comments:
Post a Comment