Thursday, August 4, 2016

Sina uhusiano na French Montana: Iggy Azalea

Wiki iliyopita rapper Iggy Azalea na French Montana walionekana pamoja huko jijini Las Vegas, walikohudhuria show ya Jennifer Lopez, Caesar’s Palace na kisha kula bata pamoja hadi asubuhi.
 
 Wakati ambapo wengi walihisi kuwa wawili hao walikuwa wakielekea kuwa na uhusiano wa kimapenzi, Iggy amekanusha tetesi hizo wakati akihojiwa kwenye E! News kwenye hafla ya 2016 Maxim Hot 100 mwishoni mwa wiki.

“No, we’re [just] collaborating,” alisema kujibu swali la kama wako pamoja kimahusiano.
“I’ve got another single coming out with French Montana, so we recorded it while I was in Las Vegas last week. It should be having a music video filmed to it in the next few weeks,” aliongeza.
Mwezi uliopita Iggy alitangaza kuachana na mpenzi wake, Nick Young baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili. Alimtuhumu Nick kwa kumpa mimba mama wa mtoto wake wa kiume.

No comments: