Thursday, August 4, 2016
Diamond athibitisha yeye ni baba kijacho, anategemea mtoto wa kiume
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ni baba kijacho, amethibitisha ujio wa Chibu Junior.
Diamond amethibitisha tetesi za ujio wa mtoto wake wa pili , ambapo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume,
“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond amefunguka kwenye kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume. Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili.”
Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, Tiffa Nassibu ambaye na umri wa mwaka mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment