Thursday, August 4, 2016

Nawaonea huruma wanao poteza muda badala ya kufanya kazi: Jibu la Joh Makini baada ya Chid Benz kusema ametengenezwa na Media

Wiki chache zilizopita Chid Benz alidai kuwa hakuna msanii wa Hip Hop ambaye amefikia mafanikio yake huku akidai Joh Makini na Nay wa Mitego wametengenezwa ili waje kulishika game la muziki.
 
Joh Makini amefunguka kuhusu kauli hiyo ambapo amesema nawahurumia watu kama hao wanaotumia muda wao kufanya mambo yasiyo ya msingi badala ya kufanya kazi.
“kusema kweli mimi hainiumizi kabisa,” Joh Makini alifunguka alipokuwa akihojiwa na Radio 5 “Kwasababu kuna vitu siviruhusu kabisa na kila mtu ana jinsi anavyoishi na Mungu wake,sana sana mimi nawahurumia watu wanaowekeza kwenye hivyo vitu,kwa sababu naona jinsi gani wana struggle kwenye kupoteza muda kuliko kufanya kazi”

Chid-Beenz_full
Kauli hiyo ya utata ya Chid Benz aliitoa alipokuwa akihojiwa na Uhuru Fm, alifunguka haya
“Sijamsikia yule mtu ambaye anafanya matukio kama mimi, yakuwa na msafara wa gari kumi, kusafiri kwenye show na watu 30, ukasikia watu 7 wamezimia kwenye show, bado sijawai kusikia matukio kama hayo labda bwana Joh Makini amefanya show Arusha wakazimia watu 9?,” alisema Chidi Benz. “Lakini nawasikia hao, kama Joh Makini namsikia na namuona kwenye muziki huu the way wametengeneza yeye ndo awe ameshika hili game, lakini hana nguvu, sisemi hivyo kama namblock hapana, hata mashabiki wake ambao wananisikiliza wamwambie nakubali hapo alipo na watu wamekutengeneza wewe ukae pale na hauna nguvu yakusema mimi ni Joh Makini, najua ni msanii mzuri lakini mimi ni The King Kong”
Aliongeza, “Kwa hiyo wapo wasanii wengi wametengenezwa, mfano Nay wa Mitego pia, ni kitu fulani kimetengenezwa. Shetta hafadhali toka ameanza kutoka alikuwa anatengenezwa ili afanye game yake,”
Chid Benz anangoma mpya ‘Chuma’ aliyomshirikisha Raymond huku Joh na yeye ana ngoma yake mpya ‘Perfect Combo’ aliyomshirikisha Chidnma.

No comments: