Friday, September 30, 2016

Hata nikila wote dini yangu sio dhambi: Diamond ajibu tetesi za kuchepuka na Hamisa mobetto na Wema kwenye remix ya All the way up

Kama ambavyo Jay Z alijibu tetesi za kuchepuka na ‘Becky with a good hair’ kwenye Remix ya All the way up baada ya mke wake, Beyonce kuachia album ya ‘Lemonade’ ndio alivyofanya Diamond.

Diamond ameachia verse ya pili ya Remix yake ya ‘All the way up’
“Mara nakula hamisa mobetto, ati Sepenga kaja magetho, ilimradi Zari apate mchecheto, Tale waambie waache unambinambi hata nikila wote dini yangu sio dhambi” Diamond arap kwenye Remix ya Hit single hiyo ya Fat Joe, Remy Ma na French Montana.
 “Siachi pengo hadi waombe poo, wao wakipost tembo si tunapost show” Huu mstari umeenda kwa nani? Mpinzani wake mkubwa Alikiba ni balozi wa Wild Aid,inayopinga mauaji ya tembo.

Mwambie na tilalila, kamwe kanzu haifanani na dera” Huu mstari ni jibu kwa Mr. Blu (Aliwahi kuimba wimbo unaitwa Tilalila), Mr. Blu aliwahi kudai Diamond amemuibia jina la Simba.

No comments: