Tuesday, September 6, 2016

Juma Jux aka African Boy aachana na utoto wa mama

Hitmaker wa ngoma ya “wivu” Jux ameiambia Tanzania kwamba zile pigo za utoto wa mama ameshatemana nazo kitambo.
Akiwa na maana kwamba kwa hivi sasa kila kitu ambacho kinahusiana na maisha yake anakisimamia yeye kama yeye tofauti na kipindi cha nyuma kipindi anaanza kazi ya muziki ambapo alikuwa anategemea pesa za nyumbani kwao ili kuendesha maisha yake ya kimuziki na hata maisha ya kawaida.
Jux ameweka wazi kwamba kipindi kile alikuwa hata akiona nguo nzuri ilikuwa akimlilia mama yake ili ampe pesa kukamilisha kile anachokihitaji, tofauti na hivi sasa ambapo muziki unamlipa kiasi kwamba umemuwezesha hadi kufungua biashaza yake mwenyewe na anaendesha maisha yake binafsi.

No comments: