Wednesday, September 9, 2020
Wednesday, April 1, 2020
Friday, March 20, 2020
Saturday, March 14, 2020
Hudson- Odoi wa Chelsea athibitisha kupona Corona (+Video)
Callum Hudson-Odoi akiwa mchezaji wa kwanza kunako Premier League kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, hatimaye hii leo siku ya Ijumaa kupitia kipande cha video amethibitisha kupona ugonjwa huo nakudfai kuwa muda si mrefu wapenzi wasoka watarajie kumuona tena uwanjani.
Mapema asubuhi Ijumaa, Chelsea ilitanga kuwa winga wake huyo alionyesha kuwa na dalili za virusi vya Corona siku ya Jumatatu. Na hivyo kikosi chote cha kwanza pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa karibu na Hudson-Odoi walilazimika kutengwa.
Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kuwa na virusi vya corona, Hudson-Odoi afya yake imeimarika na anatarajia kurejea baada ya kuumwa katika siku kadhaa.
‘’Habari zenu, kama mlivyoweza kufahamu kuwa nilikuwa na virusi siku kadhaa zilizopita, ambapo nimepona,” Hudson-Odoi amesema kupitia kipande cha video.
‘’Nafuata miongozo ya afya na kujitenga na kila mtu kwa wiki. Natumaini kuona kila mtu hivi karibuni na matumaini yangu ni kurejea uwanjani hivi karibuni.”
Friday, March 13, 2020
Thursday, March 5, 2020
Antonio Nugaz: Simba bila Janjajanja, Makandokando hawatufungi, Mwanayanga tembea kifua mbele (+Video)
Afisa Habari na Mhamasisha wa Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Young Africans, Antonio Nugaz amewahamasisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili kuishangilia timu yao huku akiongea kwa msisitizo mkubwa kuwa ‘Bila Makandokando’ Wanajangwani hao hawawezi kufungwa.
Wednesday, March 4, 2020
Friday, February 21, 2020
CAF watengua uteuzi wa Didier Drogba
Shirikisho la soka Afrika CAF kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nguli Afrika Mamadou Gaye, CAF wametengua uteuzi wa Didier Drogba kama mshauri wa Rais wa CAF Ahmad Ahmad.
July 2019 staa wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba na staa wa zamani wa Barcelona na Cameroon Samwel Eto’o waliteuliwa kuwa washauri wa Ahmad Ahmad lakini Drogba hajafanya chochote toka uteuzi huo utangazwe.
Drogba na CAF bado hawajathibitisha taarifa hizo lakini zimeenda mbali zaidi kwa kueleza Drogba toka ateuliwe hajawahi kushauri chochote kama majukumu yake yanavyotaka lakini pia hajawahi kuhudhuri shughuli yoyote ya CAF ikiwemo mechi hata moja ya AFCON 2019.
Chanzo;millardayo.com
Marioo atoboa siri alichoambiwa na Diamond walipokutana Nigeria na kuhusu kusainiwa WCB – Video
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa ngoma ya AYA @marioo_tz amefunguka kuhusu picha yake na @diamondplatnumz walipokutana nchini Nigeria.
@marioo_tz ameongeza kuwa hiyo picha ilizua gumzo sana kwa sababu hakuwa kuwa na picha akiwa na @diamondplatnumz Lakini pia walikutana wakali wawili yaani @diamondplatnumz na @marioo_tz
Pia @marioo_tz alieleza sababu za kufanya goma na @offcialcheed wa @kingsmusicrecords.
@marioo_tz ameongeza kuwa hiyo picha ilizua gumzo sana kwa sababu hakuwa kuwa na picha akiwa na @diamondplatnumz Lakini pia walikutana wakali wawili yaani @diamondplatnumz na @marioo_tz
Pia @marioo_tz alieleza sababu za kufanya goma na @offcialcheed wa @kingsmusicrecords.
Z Anto azua gumzo mtandaoni kwa kauli yake “Wasanii wakali wote wana majina ya wanyama, sijui mimi nitabatizwa jina gani mwaka huu”
Msanii wa muziki @z_antoofficial amezua gumzo mtandaoni baada ya kauli yake ‘wasanii wote wakali wanatumia majina ya wanyama’ kauli ambayo hakuifafanua zaidi.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo MakoStamina hivi karibuni akiwa katika Interviews na Bongo5TV alionyesha sana kumkubali Diamond Platnumz na kudai kwamba ni msanii mwenye mbinu nyingi za kufanya vizuri kimuziki. “Wasanii wengi wanafeli kwa kumuiga Diamond, huyu jamaa ana mbinu nyingi za kufanya muziki wake kubwa mkubwa, sasa jichanganye akupoteze” alisema Z Anto kupitia mahojiano hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)